Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2016

KUNTU YA LEO

Hivi ulishawai kujiuliza ni kwanini wanaume wengi hawapendi kuwanunulia/kuwapa zawadi (gifts) wapenzi wao? Zawadi ni nini ? Waswahili wanasema " zawadi ni zawadi " msemo huu una maana kubwa sana tena ni nzuri kama tukiuelewa vizuri Kuna tabia ya baadhi ya wanawake kukosa na kubeza zawadi wanazopewa na waume/wapenzi wao.Mwanaume anakuwa amejinyima ili ampelekee zawadi mchuchu wake,lakini matokeo yake ni kusemwa kwamba hujui kuchagua zawadi,katika zawadi na hii nayo zawadi ya kumletea mtu! Sasa mambo kama haya ndiyo yanayosababisha wanaume kuacha utamaduni wa kuwapa gifts wapenzi wao.Tambua zawadi huwa hatuchagui labda kama umeletewa zawadi ya sumu lakini vinginevyo pokea zawadi hata kama uipendi tena pokea kwa furaha tele kisha itumie japo kidogo ili umpe nguvu mtoa zawadi basi siku nyingine asikate tamaa ya kukuletea zawadi. Zawadi ina nafasi kubwa Sana katika mapenzi hata pipi pia ni zawadi. Leo nimezungumza kwa upande wa wanawake kuhusu suala la zawadi, kutu ya ...

KUNTU YA LEO

Maisha ni safari,safari ambayo ina mazuri na mabaya,magumu na mepesi.Maisha ni vile unavyoishi,suala la kufurahia maisha ni jambo linalowashughulisha wengi sana,hakuna mtu asiyependa maisha ya furaha lakini tambua huwezi kuwa na maisha furaha iliyokamilika.Furaha maana yake nini? Furaha ni kuishi unavyotaka,kufanya unachotaka na hata kupata unachotaka.Sasa kama hivi ndivyo,je kivipi unaweza kuwa na furaha iliyokamilika? Unataka uruhusiwe kufanya utakacho? Hapana huwezi kufanya tu unachokitaka ni lazima uzingatie sheria na kanuni zilizopo ama za kidini au za nchi.Hivyo huwezi kuwa na maisha yaliyojaa furaha kamili.Rizika na maisha uliyonayo lakini pambana kutafuta utakacho bila kukiuka taratibu zilizopo.