KUNTU YA LEO
Maisha ni safari,safari ambayo ina mazuri na mabaya,magumu na mepesi.Maisha ni vile unavyoishi,suala la kufurahia maisha ni jambo linalowashughulisha wengi sana,hakuna mtu asiyependa maisha ya furaha lakini tambua huwezi kuwa na maisha furaha iliyokamilika.Furaha maana yake nini? Furaha ni kuishi unavyotaka,kufanya unachotaka na hata kupata unachotaka.Sasa kama hivi ndivyo,je kivipi unaweza kuwa na furaha iliyokamilika? Unataka uruhusiwe kufanya utakacho? Hapana huwezi kufanya tu unachokitaka ni lazima uzingatie sheria na kanuni zilizopo ama za kidini au za nchi.Hivyo huwezi kuwa na maisha yaliyojaa furaha kamili.Rizika na maisha uliyonayo lakini pambana kutafuta utakacho bila kukiuka taratibu zilizopo.
Maoni
Chapisha Maoni