KUNTU YA LEO

Hivi ulishawai kujiuliza ni kwanini wanaume wengi hawapendi kuwanunulia/kuwapa zawadi (gifts) wapenzi wao?

Zawadi ni nini?
Waswahili wanasema "zawadi ni zawadi" msemo huu una maana kubwa sana tena ni nzuri kama tukiuelewa vizuri

Kuna tabia ya baadhi ya wanawake kukosa na kubeza zawadi wanazopewa na waume/wapenzi wao.Mwanaume anakuwa amejinyima ili ampelekee zawadi mchuchu wake,lakini matokeo yake ni kusemwa kwamba hujui kuchagua zawadi,katika zawadi na hii nayo zawadi ya kumletea mtu!
Sasa mambo kama haya ndiyo yanayosababisha wanaume kuacha utamaduni wa kuwapa gifts wapenzi wao.Tambua zawadi huwa hatuchagui labda kama umeletewa zawadi ya sumu lakini vinginevyo pokea zawadi hata kama uipendi tena pokea kwa furaha tele kisha itumie japo kidogo ili umpe nguvu mtoa zawadi basi siku nyingine asikate tamaa ya kukuletea zawadi.
Zawadi ina nafasi kubwa Sana katika mapenzi hata pipi pia ni zawadi.

Leo nimezungumza kwa upande wa wanawake kuhusu suala la zawadi, kutu ya kesho itakuwa jambo hili hili la zawadi lakini nitazungumza kwa upande wa wanaume. Usikose kuntu ya kesho.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

SIMULIZI YA NAKUMBUKA TU NA AWADH PALANGU

MAPENZI NI MAWASILIANO

SIMULIZI YA NAKUMBUKA TU NA AWADH PALANGU