Machapisho

MAPENZI NI MAWASILIANO

Picha
Mkumbuke mpenzi wako mara kwa mara kwa kumpigia simu,kumtumia meseji na hata kuonana naye kama inawezekana.Hii itamfanya atambue kama kweli unampenda na hata yeye ataongeza upendo na atakuwa anakukumbuka mara kwa mara.Kwa wakati wa usiku ni muhimu zaidi kumkumbuka mpenzi wako kwa mawasiliano siku hizi imezoeleka sana kuchati kwa meseji za kawaida au whatsapp itategemea lakini usimwache mpweke mpaka akafikiri hana umuhimu kwako na hii inapunguza sana mapenzi na hata kupelekea kifo kabisa cha mapenzi ya namna hii.

SIMULIZI YA NAKUMBUKA TU NA AWADH PALANGU

           NAKUMBUKA TU NA: AWADH PALANGU SIMU: 0713 899 084, 0785 056 575 2017 YALIYOMO SHUKURANIiii UTANGULIZIiv Nakumbuka tu1 SHUKURANI Kwanza ninapenda kumshukuru Allah mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniajalia siha njema na uwezo wa kuandika kitabu hiki. Nawashukuru  walimu wangu wa sarufi na fasihi kwa kunijengea msingi na kunipa maarifa yaliyoniwezesha kuandika kitabu hiki, namshukuru Mwalimu Muhango wa chuo kikuu mkwawa, Mwalimu Tito mgani mwalimu  wa kiswahili shule ya sekondari mwakavuta, wafanyakazi wa makumbusho ya Mkwawa-kalenga pia namshukuru Muslim Kalilo kwa kubuni na kuchora kifuniko cha kitabu hiki kwa usanifu. Shukurani za pekee kwa wazazi wangu na familia yangu kwa ujumla kwa mchango wao wa hali na Mali. Shukurani zangu pia nazitoa kwa wale wote waliosaidia kitabu hiki kikamilike. Allah awafanyie wepesi katika kila jamb...

SIMULIZI YA NAKUMBUKA TU NA AWADH PALANGU

           SIMULIZI- NAKUMBUKA TU MTUNZI- AWADH PALANGU SIMU: 0713 899 084, 0785 056 575 INSTAGRAM/FB AWADH PALANGU SHUKURANI Kwanza ninapenda kumshukuru Allah mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniajalia siha njema na uwezo wa kuandika kitabu hiki. Nawashukuru  walimu wangu wa sarufi na fasihi kwa kunijengea msingi na kunipa maarifa yaliyoniwezesha kuandika kitabu hiki, namshukuru Mwalimu Muhango wa chuo kikuu mkwawa, Mwalimu Tito mgani mwalimu  wa kiswahili shule ya sekondari mwakavuta, wafanyakazi wa makumbusho ya Mkwawa-kalenga pia namshukuru Muslim Kalilo kwa kubuni na kuchora kifuniko cha kitabu hiki kwa usanifu. Shukurani za pekee kwa wazazi wangu na familia yangu kwa ujumla kwa mchango wao wa hali na Mali. Shukurani zangu pia nazitoa kwa wale wote waliosaidia kitabu hiki kikamilike. Allah awafanyie wepesi katika kila jambo la kheri. UTANG...

KUNTU YA LEO

Hivi ulishawai kujiuliza ni kwanini wanaume wengi hawapendi kuwanunulia/kuwapa zawadi (gifts) wapenzi wao? Zawadi ni nini ? Waswahili wanasema " zawadi ni zawadi " msemo huu una maana kubwa sana tena ni nzuri kama tukiuelewa vizuri Kuna tabia ya baadhi ya wanawake kukosa na kubeza zawadi wanazopewa na waume/wapenzi wao.Mwanaume anakuwa amejinyima ili ampelekee zawadi mchuchu wake,lakini matokeo yake ni kusemwa kwamba hujui kuchagua zawadi,katika zawadi na hii nayo zawadi ya kumletea mtu! Sasa mambo kama haya ndiyo yanayosababisha wanaume kuacha utamaduni wa kuwapa gifts wapenzi wao.Tambua zawadi huwa hatuchagui labda kama umeletewa zawadi ya sumu lakini vinginevyo pokea zawadi hata kama uipendi tena pokea kwa furaha tele kisha itumie japo kidogo ili umpe nguvu mtoa zawadi basi siku nyingine asikate tamaa ya kukuletea zawadi. Zawadi ina nafasi kubwa Sana katika mapenzi hata pipi pia ni zawadi. Leo nimezungumza kwa upande wa wanawake kuhusu suala la zawadi, kutu ya ...

KUNTU YA LEO

Maisha ni safari,safari ambayo ina mazuri na mabaya,magumu na mepesi.Maisha ni vile unavyoishi,suala la kufurahia maisha ni jambo linalowashughulisha wengi sana,hakuna mtu asiyependa maisha ya furaha lakini tambua huwezi kuwa na maisha furaha iliyokamilika.Furaha maana yake nini? Furaha ni kuishi unavyotaka,kufanya unachotaka na hata kupata unachotaka.Sasa kama hivi ndivyo,je kivipi unaweza kuwa na furaha iliyokamilika? Unataka uruhusiwe kufanya utakacho? Hapana huwezi kufanya tu unachokitaka ni lazima uzingatie sheria na kanuni zilizopo ama za kidini au za nchi.Hivyo huwezi kuwa na maisha yaliyojaa furaha kamili.Rizika na maisha uliyonayo lakini pambana kutafuta utakacho bila kukiuka taratibu zilizopo.